ACHENI KUCHUKULIA CHANGAMOTO KAMA SABABU YA KUTOKUWAJIBIKA

Posted on: February 29th, 2024

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Ibenzi Ernest amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo vyote ndani ya Hospitali kusimamia uwajibikaji kwa watendaji wote na kuwataka kuacha Tabia ya kuchukulia uwepo wa baadhi ya changamoto zinazojitokeza kama sababu ya kutokuwajibika

Ameyasema hayo februari 29, 2024 akiwa katika kikao kazi na wakuu wa idara na vitengo, ambapo amesema uwajibikaji ni pamoja na kutatua changamoto kwa wakati ili kuleta matokeo chanya.

'Tuache kuchukulia uwepo wa baadhi ya changamoto kama sababu ya kutotimiza majukumu yetu ipasavyo, kwa kufanya hivyo ni uzembe kama ulivyo uzembe mwingine " amesema Dkt Ibenzi