Hospitali Rufaa Dodoma wapokea magari ya wagonjwa

Posted on: May 3rd, 2020

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dodoma (RRH) wamepokea msaada wa gari la kubeba wagonjwa kutoka asasi ya Australia Tanzania Society (ATS) kupitia Rafiki Surgical Missions.

Akipokea msaada huo, kwa niaba ya  uongozi wa hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura wa MNH, Dkt. Juma Mfinanga amesema msaada huu umekuja wakati mzuri kwani matumizi ya gari hilo utaisaidia Hospitali ya Mkoa kukabiliana na changamoto ya wagonjwa wa dharula

Kwa upande wa mwakilishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Bw. Maxmillian Tryphone ameshukuru kupatiwa msaada huo kwani itasaidia kwa kiwango kikubwa katika kuendesha shughuli za matibabu hospitalini hapo.

Naye Mkurugenzi wa ATS Bw. James Chialo amesema leo amekabidhi magari hayo na kufikisha idadi ya magari sita ambayo wameshatoa msaada nchini na kuna magari kama hayo 10 wataleta na kuyasambaza nchini ili kusaidia sekta ya afya.

Amesema ATS kupitia Rafiki Surgical Missions kila mwaka wamekua wakileta watalaamu wa upasuaji ili kushirikiana na watalaamu wa hapa nchini kufanya aina mbalimbali za upasuaji.

Balozi wa ATS, Bw. Banana Zoro amesema amekuwa akifanya kazi na asasi hiyo katika kusaidia sekta ya Afya nchini na kwamba ni jambo zuri kushiriki katika shughuli ya utoaji wa msaada huo.