Ukaribisho

profile

DR.IBENZI ERNEST
Mganga Mfawidhi

"Karibu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Hospitali yetu ipo katikati ya Jiji la Dodoma .Hospitali yetu hutoa huduma mbalimbali pamoja na huduma za kibingwa kama ifuatavyo,Huduma za Mifupa,upasuaji mkubwa,Magonjwa ya ndani,huduma ya watoto,huduma za Mama na Mtoto,Afya ya Meno na Kinywa,Tiba ya viungo saidizi,Tiba kwa vitendo,pamoja na huduma za kibingwa pia tunatoa huduma za chanjo ambazo ni chanjo ya homa ya Ini  (Hepatitis B Vaccine) na chanjo ya homa ya manjano (Yellow fever vaccin ).Katika Hospitali yetu tunayo Maabara kubwa na ya kisasa kabisa inayotoa huduma mbalimbali .Huduma zoote zipatikanazo katika Hospitali yetu hutolewa kwa huduma ya bima na huduma ya kulipia papo kwa papo na pia tunazingatia sera ya Afya ya Taifa kwa kutoa huduma kwa makundi maalumu. Hospitali inawakaribisha kupata huduma rafiki.